Mwanamke anayejulikana kwa jina la Tatu Ikoko akitishia kusaula mbele ya watu.
HATARI!
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu Ikoko mkazi wa
Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa kutembea bila
nguo baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke mwingine.
“Alitoka usiku mzima akarudi saa moja
asubuhi akamkuta bwana’ke yuko na mwanamke mwingine ndani, akaanzisha
vurugu, akavua nguo na kubaki na kanga moja na kuanza kupita mtaani huku
akisema nivue nisivue na watu wakawa wanamuitikia vua.
Tatu Ikoko akiwa katika hali ya kuvurugwa baada ya kumfuma mumewe na hawara.
“Baada ya hapo tu watu wazima na mashosti zake walimshika na
kumsitiri, akaja bwana’ke akamchukua wakaenda nyumbani kwao,” kilisema
chanzo hicho.
Chanzo kiliendelea kufunguka kuwa tukio
hilo siyo mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kwani alishawahi kufanya
hivyo akiwa na mwanamume mwingine aliyejulikana kama Kisiso mtaani hapo
na waliachana kwa tabia hiyo.
Majirani wakimsitiri Tatu Ikoko.
“Akiwa na mwanaume halafu akamfumania, ndiyo huwa anafanya hivi na
yule mshikaji wa kwanza kwa aibu ilibidi ahame, sasa hivi anaishi
Mbagala,” kilisema chanzo hicho.imeandikwa na shani ramadhani na mayasa
mariwata.
CREDT-GPL
0 comments:
Post a Comment