Kuwepo
kwa mitandao ya kijamii kumeleta mambo mengi na mengine sio ya kawaida
mfano tabia iliyopo siku hizi ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakianzisha
uhusiano mpaka wa kimapenzi kupitia mitandao hiyo na hawajawahi
kukutana kabla, wapo wachache ambao wameweza kuvuka na kufikia hatua ya
kuoana lakini wengi huishia barabarani.
“Wewe sio mwanamke niliyekuwa nakufikiria.. samahani, ila ninakuacha”
bwana harusi alisikika akisema hayo maneno siku ya ndoa baada ya
kukutana uso kwa uso na bibi harusi siku ya ndoa yao huko Saudi Arabia.
Wageni waalikwa walishtuka na bibi
harusi akapoteza fahamu huku ndugu na jamaa wakimsihi jamaa akubali ndoa
hiyo iendelee, utamaduni wa nchi za mashariki ya kati, magharibi mwa
Madina wapenzi huweza kuoana hata bila kufahamiana.
Bwana harusi huyu alimpa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona
uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha alipotaka kuwapiga
picha, maharusi hawa kutoka mji wa magharibi wa Saudia,Medinah
walikubaliana kuoana licha ya kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni
utamaduni mkubwa wa mataifa ya mashariki ya kati.
Unaambiwa Mwanamke huyuo alipofungua kitambaa alichokuwa amejifunika
uso na kutabasamu kwenye camera, mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla
ambapo kwa mujibu wa gazeti la Okaz, mwanamume huyo alianguka na
kuzirai.
Hata hivyo Bwana harusi aliliambia gazeti hilo kwamba hakuweza
kumwona bi harusi kabla ya harusi ambapo kauli zake ambazo haziwezi
kusahaulika ni hizi >>> ”Si wewe msichana niliyetaka kuoa, si wewe kamwe niliyedhani kwa hivyo nakupa talaka’
Kingine kikubwa kilichoripotiwa ni
kwamba baada ya Bibi Harusi kupewa talaka alianguka na kuzirai na
kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.
CREDT-MILLARDAYO
0 comments:
Post a Comment