Jumamosi Ya Nov 29 2014 Watanzania na wapenzi wa muziki wa bongo fleva walifuatilia kwa karibu sana tuzo za Video za Channel O zilizofanyika Johannesburg South Africa. Mtanzania mwenzetu Diamond Platnumz alikuwa akiwania tuzo nne kwenye vipengele tofauti.
Diamond Platnumz amefanikiwa kushinda tuzo tatu kati ya 4alizokuwa anawania. Tuzo alizoshinda ni Most Gifted EastAfrica, Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer.
Hizi ni picha za Diamond akiwa na mama yake mzazi, manager wake Bab Tale na Said Fela na Zari kutoka Uganda.
“Kiukweli,
haikuwa rahisi kabisa.. lakini kwa uwezo wa Mwenyez Mungu na support
kubwa mliyonipa iliwezesha Bongo Flavour yetu kuandika Historia mpya
kwenye Ramani ya mziki wa Africa…Hii inaonyesha ni jinsi gani Umoja ni
nguvu na pia jins gani mziki wetu ukisupportiwa na kupewa kipaumbele
unaweza kufika mbali zaidi… Shukran sana kwa @channeloafrica @channelotv
kwa kuniona na kuthamini kipaji changu, My Family, Management, Media
zote zilizokuwa zikinisupport, Watangazaji, Wasanii, Wadau na bila
kuwasahau wapendwa wangu #TeamWasafi #TeamChibu #TeamPlatnumz #TeaMMondi
toka instagram, Facebook, Whatsapp, Twitter na kadharika, wakiongozwa
na kamanda langu @kifesi … Nawashkuruni sana sana
0 comments:
Post a Comment