Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Oakland, California. Mwesigwa Blandesi. Marehemu ndiye aliyekuwa ananialika kwenye shughuli nyingi nilizokuwa nafanya California. KWETU Fashions inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu , marafiki na jamaa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. Daima tupo pamoja kwenye msiba huu mkubwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awatie nguvu. Roho ya marehemu ipumzike kwa Amani,
.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Oakland, California. Mwesigwa Blandesi. Marehemu ndiye aliyekuwa ananialika kwenye shughuli nyingi nilizokuwa nafanya California. KWETU Fashions inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu , marafiki na jamaa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. Daima tupo pamoja kwenye msiba huu mkubwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awatie nguvu. Roho ya marehemu ipumzike kwa Amani,
Posted by kifesi |
Mwanaharakati, mshairi na mwandishi mahiri wa vitabu duniani Maya Angelou amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.
Ikiwa ni moja katika ya sauti kubwa za kifasihi duniani, Maya alitengeneza jina lake mwaka 1969 kupitia kitabu cha I Know Why the Caged Bird Sings.
maya
Familia yake imesema kuwa Mwanaharakati huyo aliishi kama mwalimu, mwanaharakati,msanii na mtu mwenye utu. Alikuwa sauti ya amani duniani.
Maya amefariki akiwa nyumbani kwake Kaskazini mwa Jimbo la North Carolina.
Posted by kifesi |
Mwigizaji maarufu wa filamu wa nchini Marekani Angela Basset anatarajia kuongoza filamu itayohusu maisha halisi ya aliyekuwa mwanamuziki nguli duniani Witney Houston. Kituo cha Televisheni cha Lifetime cha Marekani kimethibitisha kuwa filamu hiyo itaelezea maisha ya Witney hadi kuibukia kwenye umaarufu pamoja na mahusiano yake na aliyekuwa mume wake kwa kipindi hicho Bobby Brown kuanzia mara ya kwanza walipokutana hadi kufunga ndoa. Mwanamuziki Witney Houston alifariki dunia February mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 48. Witney alikutwa amekufa chumbani kwake katika hoteli jijini Los Angeles. Angela Basset amecheza filamu nyingi zinazohusu maisha halisi ya watu ambapo pia aliwahi kucheza filamu ya hayati Notorious BIG akiwa kama mama yake na kutumia jina la Voletta Wallace.
Subscribe to:
Posts (Atom)